Aunty Ezekiel afunguka kuhusu Kutarajia Mtoto wake wa Pili

Zile tetesi za muigizaji wa filamu nchini Aunty Ezekiel ni mjamzito huenda zikawa zimetimia baada ya kuficha kwa muda mrefu.
Akiongea kwenye kipindi cha FNL cha EATV, Aunty hajaweka wazi kama ni kweli ni mjamzito ila alichokisema ni kuwa anatamani tena kupata mtoto mwingine wa kike baada ya mtoto wao wa kwanza Cookie naye kuwa wa kike.
“I wish nipate mtoto wa kike tena, watoto wa kike hela ile, yaani mpaka wajae,” amesema muigizaji huyo.
Aunty Ezekiel ameongeza kuwa hataki kuweka wazi kama ni mjamzito kwa sasa ila watu watafahamu tu kwa kuwa hata mimba yake ya kwanza aliificha lakini watu waliweza kuibaini.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment