Diamond kumleta hasimu wa Zari kwenye Wasafi Beach PartyDiamond Platnumz ni mfanyabiashara kwenye muziki asiyeogopa ‘kutake risk’ kwaajili ya kukamilisha azma yake, hata kama uamuzi atakaouchukua unaweza ukaleta mzozo ndani ya familia yake.
Katika kunogesha tamasha lake kubwa la Wasafi Beach Party, hitmaker huyo anamdondosha hasimu mkubwa wa mchumba wake Zari, Huddah Monroe. Kama umesahau, Huddah aliwahi kuingia kwenye bifu kali na Zari baada ya kudai kuwa amewahi kutembea na Diamond na kwamba staa huyo ni ‘mali ya umma.’
Diamond ameweka picha ya mrembo huyo kwenye Instagram akiwa ameipa kamera mgongo na kuwataka mashabiki wake kubashiri ni nani.

Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment