Profesa Joyce Ndalichako azitaja changamoto zinazoikabili sekta ya elimu

Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako ametaja moja ya changamoto zinazokabili sera ya elimu msingi bure, kuwa ni upungufu wa fedha za kila mwezi zinazotolewa, kutotosheleza kulipia mahitaji ya msingi kama umeme, maji ambavyo mwanzoni vilikuwa vikilipiwa na wazazi.

Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako.
Aliyasema hayo Jumatano hii wakati akizungumza na ujumbe wa Benki ya Dunia uliongozwa na Meneja wa Utendaji Elimu anayesimamia nchi za Mashariki na kusini mwa Afrika, Sajitha Bashir.
Mazungumzo hayo yalifanyika Jumanne hii jijini Dar es Salaam. Katika mazungumzo yao, Profesa Ndalichako alisema Sera ya Elimu ya Msingi bure tangu kuanza kutekelezwa imekuwa na ongezeko kubwa la uandikishaji wa wanafunzi katika elimu ya awali na msingi.
“Ongezeko hii limekuja na changamoto kadhaa ambazo Serikali inazifanyia kazi ili kuweza kuzitafutia ufumbuzi,” alisema Profesa Ndalichako ambaye aliishukuru Benki ya Dunia kwa kufadhili miradi mingi katika sekta ya elimu na nia yake ya kuendelea kufadhili miradi mingine katika sekta hiyo.
Aidha Ndalichako alisema lengo la serikali ni kuhakikisha nchi inakuwa na wananchi wenye maarifa, stadi, uwezo na mtazamo chanya unaongeza thamani katika maendeleo ya nchi.
Sambamba na kutaja changamoto nyingine hizo alisema pia changamoto nyingine ni upungufu wa miundombinu ya madarasa, vyoo na mahitaji mengine ya kujifunzia na kufundishia na wanafunzi wengine wanatembea mpaka kilometa tatu kufuata shule.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment