Profesa Mukandala aongezewa muda UDSM

Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) ambaye ni Rais mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Mrisho Kikwete baada ya mashauriano ameafikiana na Rais John Magufuli kuongeza muda wa Makamu Mkuu wa chuo hicho wa sasa, Profesa Rwekaza Mukandala kwa muda wa mwaka mmoja.


Katika taarifa aliyoituma kwa vyombo vya habari Jumatatu hii, Mwenyekiti wa Baraza la chuo hicho, Peter Ngumbullu alisema uamuzi huo unaanza mara moja huku akisema kuwa muda wa profesa huyo ulimalizika Disemba 4 mwaka huu.
Profesa Mukandala alisema alikuwa ameshajitayarisha kwamba juzi angekabidhi madaraka hayo kwa mtu mwingine, lakini kwa imani waliyokuwa nayo uongozi wa chuo hicho uliridhia aendelee kwa mwaka mwingine.
“Viongozi wa chuo hiki wakishirikiana na Rais John Magufuli wamekuwa na imani na mimi na kuniongezea mwaka,” alisema Profesa Mukandala.
Aidha Profesa Mukandala ameahidi kuendelea kufanya kazi kwa kushirikiana na viongozi wote na jumuiya ya wanachuo ili UDSM iendelee kuwa bora. Pia alisema ataendelea kuenzi na kutunza tunu ya chuo hicho iliyoachwa na Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere.
Profesa Mukandala aliteuliwa kwa kipindi cha miaka mitano kilichoanza Desemba 5, 2011.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment