Tangu nimefunga ndoa, sioni tabu naona raha tu – Mwana FA

Msanii wa muziki wa hip hop, Mwana FA amesema anayafurahia sana maisha ya ndoa tofauti na inavyodhaniwa na vijana wengi wenye uoga wa kuingia katika maisha hayo
Rapa huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo Dume Suruali, amedai toka aingia kwenye maisha ya ndoa amekuwa ni mtu mwenye furaha zaidi.
“Ndoa siyo ngumu kama inavyofikiriwa na wengi, cha msingi muelewane, kila mtu ajue unachofanya, na kuheshimu nafasi yake ndani ya ndoa, maisha ya ndoa ni mzuri sana, tangu nimefunga ndoa, sioni tabu naona raha tu,” Mwana FA alikiambia kipindi cha FNL cha EATV wiki hii.
Mkali huyo wa wimbo ‘Bado Nipo Nipo’ aliyoitoa takriban miaka 7 iliyopita iliyokuwa ikitisha vijana kuoa, amedai aliyoyaimba katika ngoma ile ni ya kweli, na yalimsaidia kufanya utafiti wa kutosha kabla ya kuingia kwenye ndoa na ndiyo maana ndoa yake haina mambo kama yale aliyoyaimba katika ngoma ile.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment