Watanzania wengi walitumia Google kutaka kujua maana ya ‘Bae'

Tuwalaumu Sauti Sol na Alikiba kwa wimbo wao ‘Unconditionally Bae’ kiasi cha kuwafanya watanzania wengi kukimbilia Google kutaka kujua maana yake ama ni kwasababu wapendanao wamelifanya neno hilo maarufu zaidi mtandaoni kwa jinsi wanavyoitana kwenye Instagram?

Well, ni ngumu kujua jibu, lakini kwa mujibu wa ripoti za Google, Bae ni neno la tatu ambalo Watanzania wengi wameliandika kwenye search engine hiyo kutaka kujua maana yake. Kama nawe ni mmoja wa watu ambao huliona sana neno hilo lakini hujui linamaanisha nini, Bae ni kufupi cha baby, neno ambalo wapenzi huitana kwa huba!

Tovuti ya BBC Swahili, imeandika ripoti ya Google ya mwisho wa mwaka kuonesha ni maneno gani ambayo yalitafuta zaidi kwenye mtandao huo.
Hivi ndivyo mambo yalivyokuwa:
Vitu vilivyotafutwa zaidi:
1.matokeo ya darasa la saba 2016
2.beka boy
3.mkekabet
4.salehe jembe juni 26 2016
5.Malazi Arusha
6.euro 2016
7.matokeo ya kidato cha nne 2016
8.yinga media
9.muungwana
10.Raymond
Walichotaka kujua sana kufanya:
Jinsi ya kuweka tone la dawa jichoni
Jinsi ya kupata wawekezaji/wafadhili
Jinsi ya kukuza nyusi
Jinsi ya kujua tarehe ya kujifungua
Jinsi ya kuacha kukoroma
Jinsi ya kufanya cd kuweza kuifungulia kompyuta
Jinsi ya kuomba na ubani
Jinsi ya kupika danish na croissant
Jinsi ya kuanzisha kiwanda cha chokoleti
Jinsi ya kujua iwapo mtoto amegeuka
Ni nini:
Furaha kamili/upeo wa furaha ni nini
Malengo ni nini
Bae maana yake ni nini
Elimu rasmi ni nini
Ndoa ya wake wengi ni nini
Hesabu ya jumla ni nini
Matumizi ya pesa ni nini
Soko la kubadilishana sarafu za kigeni ni nini
Mfumo ni nini
Ghala ni nini
Ripoti thanks to Bongo5
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment