Watendaji wa halmashauri waficha taarifa za kipindupindu kuogopa kutumbuliwa

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amesema kuna baadhi ya halmashauri nchini zimekuwa zikificha taarifa za Kipindupindu kwa kuogopa kuchukuliwa hatua na Rais Dkt John Magufuli.


“Kuna baadhi ya halmashauri zinaficha taarifa za wagonjwa wa kipindupindu kwa kuogopa kutumbuliwa na mheshimiwa Rais. Kwasababu mheshimiwa rais alisema kuwa wakuu wa wilaya na wakurugenzi ambao kwao kutakuwa na njaa, kipindupindu, atawachukulia hatua. Kwahiyo matokeo yake watu wamekuwa wakificha taarifa, na inasikitisha sana unakwenda katika hospitali unakuta wagonjwa wa kipindupindu wamechanganywa na wagonjwa wengine,” alisema Waziri Ummy wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mlipuko wa ugonjwa wa Kipindupindu katika baadhi ya maeneo nchini.
“Hili si suala tu la kukiuka maadili lakini ni sawa sawa na mauaji, ni kosa la jinai, ndio maana kwa kupitia kwenu nawatahadharisha viongozi wote wa halmshauri kutoa taarifa za wagonjwa wa kipindupindu. Kutoa taarifa inatusaidia na inasaidia mkoa na halmashauri kuchukua jitihada mbalimbali za kuchukua hatua,” aliongeza
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment