WHO yadai hakuna ugonjwa wa Zika nchini

Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema hakuna taarifa za ugonjwa wa Zika nchini Tanzania na hakujawahi kupatikana mtoto aliyezaliwa na dalili hizo.


Hayo yamesemwa na Mwakilishi wa shirika hilo nchini Tanzania, Dk Grace Saguti alipozungumza na waandishi wa habari.
“WHO inafanya kazi na wizara ya afya kufuatilia taarifa za magonjwa unaofanyika kila siku katika maeneo yote ya afya, na taarifa huletwa wizarani kisha tunashirikishwa ili kutoa katika tovuti yetu, nachoweza kusema hatujapata taarifa za magonjwa ambazo zinazoonyesha dalili za mgonjwa yoyote mwenye zika Tanzania,” amesema Dk Saguti.
Pia, Mganga Mkuu wa Serikali, Dk Mohamed Kambi amesema Wizara ya Afya ina mfumo maalum wa kupata taarifa za magonjwa na hakuna taarifa iliyoonyesha uwepo wa ugonjwa wa zika “Hakuna mgonjwa yoyote wa Zika Tanzania, narudia mara ya pili hakuna mgonjwa wa zika Tanzania.”
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment

Note: only a member of this blog may post a comment.