Zitto Kabwe na mkewe wapata mtoto wa kike

Mwenyekiti wa chama cha ACT wazalendo, Zitto Kabwe amefanikiwa kupata mtoto wa kike. Mtoto huyo amezaliwa saa 1 na dakika 45 asubuhi leo, Disemba 27 mwaka 2016
Hii ni taarifa yake:
Mimi na Mke wangu mpendwa tumebarikiwa na Allah kupata mtoto wa kike. Mtoto na mama yake wana afya njema kabisa, Mashaallah. Mtoto amezaliwa saa moja na dakika 45 asubuhi leo Disemba 27, 2016.
Binti yetu ataitwa Josina – Umm Kulthum. Josina kwa heshima ya mwanamama mpigania Uhuru wa Kusini mwa Afrika, Josina Muthembi Machel wa FRELIMO. Umm Kulthum kwa heshima ya mama yangu mdogo na pia jina la binti wa Mtume Muhammad (SAW)
Tunamshukuru mungu kwa Baraka hizi za mtoto Josina – Umm Kulthum Zitto.
Kabwe Z. Ruyagwa Zitto
Disemba 27, 2016
Dar Es Salaam

Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment