Alikiba siyo bwana wangu na wala hajawahi kuwa bwana wangu – Queen Darleen

Msanii wa muziki kutoka WCB, Queen Darleen amekanusha uvumi ambao waliwahi kusambaa kwenye mitandao ya kijamii kuwa alikuwa anatoka kimapenzi na msanii Alikiba.

Muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo Kijuso, amesema mara nyingi watu wakiona anakuwa karibu na mtu fulani huwa wanahisi kuwa ni mtu wake.
“Alikiba siyo bwana wangu na wala hajawahi kuwa bwana wangu, ila Alikiba alikuwa mshikaji wangu na zaidi ya mshikaji wangu, yaani ni ndugu kabisaa, hivyo watu waliweza kuona natoka naye kwa kuwa nilikuwa karibu naye, nazunguka naye mara kwa mara karibu sehemu zote, hivyo watu wakawa wanajua hivyo na hiyo ni kutokana na ukweli kwamba watu walikuwa hawamjui bwana wangu.” Queen Darleen alikiambia kipindi cha Enewz cha EATV.
Muimbaji huyo alizidi kufafanua na kusema kama kweli angekuwa anatoka kimapenzi na Alikiba kipindi hicho basi hata mtoto wake angekuwa ni mtoto wa Alikiba.
“Kipindi kile nazurula sana na Alikiba mimi nilikuwa tayari mjamzito, na nisha jifungua na mtoto kwa mantiki hiyo kama Alikiba angekuwa bwana wangu basi yule mtoto angekuwa wa Alikiba, lakini mimi nilikuwa na mwanaume wangu kipindi hicho ambaye ni Hamisi Dakota hivyo watu wanaotujua sisi walikuwa wanajua jinsi gani tunavyoishi, Mimi nilishaambiwa hata Dully Skyes bwana wangu wakati yule ni kaka yangu, ikaenda wakati Nassibu anaanza kutoka nilikuwa naye karibu katika kumsaidia kazi zake watu wakasema kuwa bwana wangu” aliongeza Queen Darleen
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment