Mtanzania huyu ajipatia umaarufu Youtube kwa simulizi yake ya jinsi alivyokutana na mume mzungu

Victoria David, si msanii wa muziki ama muigizaji wa filamu. Ni msichana mwenye maisha ya kawaida tu lakini aliyejipatia umaarufu Youtube.


Channel yake hadi sasa ina subscribers zaidi ya elfu tano. Si mchezo kufikisha idadi hiyo hasa kama haupo kwenye showbiz. Ni kwanini Victoria amepata umaarufu huo? Well, ni simulizi yake ya ukweli ya mapenzi ya namna alivyokutana na mume wa kizungu anayedai amebadilisha maisha yake na kuishi ndoto zake.
Ni simulizi ya kuvutia, no wonder imevutia watu wengine, akiwa na uwezo wa kupata zaidi ya views elfu 10 kwa siku kila akiweka video mpya. Na hakika, Victoria anaweza kuwa mfano wa namna ambavyo watu wa kawaida wenye visa vya kusisimua wanaweza kujipatia si tu umaarufu, bali pia kipato kupitia Youtube.
Pamoja na kusimulia mkasa wake, Victoria ambaye anaishi ughaibuni na mumewe, huitumia channel yake kuzungumzia masuala ya urembo.

Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment