Mume amuuwa mke wake kisa kachumbari na kupika mboga isiyo na kiwango

Mkazi wa mtaa wa Mageuzi, kata ya Ngokolo, Shinyanga, Ibrahimu Daniel (42) amemuua mke wake, kwa kushindwa kuhifadhi vizuri kachumbari na kupika mboga isiyo na kiwango.

Aliyeuawa ni Stella Ibrahimu (39) na alipigwa baada ya mumewe Daniel kurudi nyumbani na kuuliza kachumbari ambayo alikula jana yake ndipo mtoto aliyekuwa akimlea Elizabeth Ibrahimu (13) alipomuonesha, lakini hakuridhika nayo na kuanza kuuliza maswali kwa nini haikuhifadhiwa vizuri.
Waandishi wa habari waliofika eneo la tukio walielezwa na mtoto wa marehemu, Daniel Ibrahimu (12) kuwa baba yake alipofika nyumbani saa moja usiku alimkuta yeye akiwa na Elizabeth ndipo alipoanza kumhoji Eliza akimuuliza kachumbari yake iko wapi.
Daniel alisema baada ya Eliza kumuonesha baba yake kachumbari hiyo aliyoila na kuibakisha Jumatatu wiki hii, aliiona imechacha na kuonekana na uchafu, ndipo alitoka nje na kuchukua fimbo anayoihifadhi juu ya nyumba na kutaka kuanza kumpiga lakini kabla ya kumpiga mtoto huyo alichoropoka na kukimbia nje.
Aliendelea kusimulia kuwa baada ya kukimbia na binti huyo, mama yake ambaye alikuwa kazini alifika nyumbani wakati huo mfarakano ukiendelea na alimkuta baba yao akifoka na baada ya kuuliza kuna nini, aliambiwa kwa nini hakupika mboga yenye kiwango na kwa nini alipika ugali mwingine wakati kulikuwa na ugali uliobaki mchana.
“Mama alifika na kuanza kunywa chai lakini baba aliendelea kufoka ndipo mama alimjibu kwa hasira ndipo alipomuuliza baba uliacha fedha ya matumizi ya kuweza kupika mboga yenye kiwango, alianza kumpiga baadaye alimpiga na kikombe na mateke akaanguka ndipo mimi nilikimbia kwa majirani kuwataarifu mama anapigwa, walikuja na kukuta mama ameanguka chini baba akiwa anamruka ruka,” alisema Daniel.
Majirani waliofika katika tukio hilo, Gloria Shija na Retisia Mashalah, walisema, walikuta baba huyo amefunga mlango na walipomgongea afungue, alikataa, lakini baada ya kuchungulia dirishani walimuona anampuliza puani na masikioni huku akimmwagia maji ili azinduke, baada ya kuona hazinduki, Shija anasema walipofanikiwa kuingia ndani walimbeba marehemu na kumpeleka hospital lakini walikuta tayari amefariki.W
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment