Najipanga kuwaachia vijana muziki niingie kwenye siasa – Asha Baraka

Mkurugenzi na mmliki wa bendi kongwe ya muziki wa dansi nchini Twanga Pepeta, Asha Baraka amedai yupo mbioni kuachana na maswala ya muziki na kujikita kwenye siasa.

Asha Baraka amedai tayari ameshafanya kazi kubwa kwenye muziki wa dansi na muda huu ni kwa ajili ya vijana na yeye aingie kwenye siasa.
“Muziki unakuwa kwa kasi sana japo kuwa bado kuna changamoto nyingi kama unavyojua, media nyingi hazipigi nyimbo za muziki wa bendi kwa uwiano sawa na nyimbo za aina zingine za muziki. Kwa hiyo media zibadilike kwa sababu sisi wengine tunajipanga kuwaachia vijana na kuingia kwenye siasa,” Asha Baraka alikiambia kipindi cha NFL cha EATV.
Pia alisema anaamini wizara yenye dhamana na maswala ya burudani itafanya juhudi za kusaidia kuurudisha muziki wa dansi katika chati kwa mwaka 2017.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment