Pale Stereo ampigia magoti Chemical kumuomba penzi

Msanii wa muziki wa hip hop Stereo ambaye siku za karibuni alitangaza wazi nia yake na hisia zake juu ya kuhitaji kwa udi na uvumba penzi la Chemical, Ijumaa hii akitutana live na mwanadada huyo na mkumpigia magoti kueleza kile kinachomsibu moyoni mwake.


Rapa Stereo akipiga magoti kumuomba Chemical akubaliane na ombi lake.
Rapa huyo alikukutana na Chemical katika kipindi cha Friday Night Live cha EATV na kuamua kuitumia nafasi hiyo kumchana kile kinachomsibu.
“Nathubutu kusema ukweli mbele ya umati wa watu wanaotazama hapa muda huu na ambao wanasikiliza kupitia redio wanaona na kunisikia kijana ambaye nampenda Chemical,” Stereo alisema akiwa amepiga magoti pamoja na kumshika mkono mrembo huyo.
“Hii sio siri tena Umma mzima utambue, nipo serious,” aliongeza.
Baada ya kauli hiyo, Chemical alisema “Nimeshakusikia” huku akidai hajawai kupitia experience ya mwanaume kumtokea live namna hiyo
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment