Ray Kigosi atarajia kupata mtoto wa kwanza kutoka kwa mpenzi wake Chuchu Hans

Msanii mkongwe wa filamu nchini, Vicent Kigosi ‘Thegreatest’ anatarajia kupata mtoto wake wa kwanza kutoka kwa mpenzi wake ambaye pia ni msanii wa filamu, Chuchu Hans.


Muigizaji huyo amedai mahusiano yao yamepitia vikwazo vingi mpaka kufikia hatua waliyofikia sasa.
“Kwanza kabisa napenda kumrudishia sifa na utukufu mungu baba muumba wa mbingu na ardhi tumepitia vingi vikwazo lakini yeye atutiaye nguvu aliendelea kusimama na sisi imara asante sana mungu kwa kuwa mwema kwetu mengi yalisemwa juu yetu lakini mungu baba umejibu ulikuwa mwezi mmoja kama utani vile hatimaye imefika miezi tisa na sasa kubaki siku chache nakuombea my lovely mzungu, Mungu akufanyie wepesi,” aliandika muigizaji huyo kupitia instagram.
Muigizaji huyo alikuwa kimya kwa muda mrefu kuzungumzia ishu ya mahusiano yake na Chuchu Hans

Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment