TAARIFA YA DUA YA HITMAH YA MZEE WETU HAMADI KILUVIA.

Familia ya marehemu Hamadi Kiluvia inapenda kutoa shukrani  zao za dhati kwa ndugu jamaa na marafiki kwa ushirikiano wenu mkubwa  mliouonyesha katika msiba wa baba yao mpendwa Hamadi Kiluvia ambaye alifariki dunia mnamo tarehe 23/11/2016.
Familia inapenda kuwashukuru kwa ushirikiano wao Raisi Mstaafu Dr Jakaya Kikeete,Waziri Mkuu mstaafu Cleopa Msuya, Naibu Speaker Dr Tulia Ackson, Mbunge wa Chalinze muheshimiwa Ridhiwani Kikwete na viongozi wengine wa mbalimbali wa Serikali walioweza kufika na kushirikiana nao katika msiba wa baba yao. 
Tunapenda pia kuwashukuru IPP media, Clouds Raido, Groove Back Entertainment, Misokia Catering , Uongozi wa Yanga na TFFA.
Familia pia inapenda kutoa shukrani zao kutoka Moyoni kwa wote mlioshiriki katika msiba huu
Dua;
Famila ya marehemu mzee Hamadi Kiluvia inapenda kuwakaribisha kwenye hitmah Dua ya kumaliza msiba itayofanyika nyumbani kwa marehemu no 93 Regent Estate migombani road  Siku ya tarehe  07/01/2017 saa 7 mchana .
Kwa maelezo zaidi piga no 0768768284 or 0657755555

Asanteni sana Mungu awabiriki

Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment