Talaka na Gardner ni moja ya mambo 4 aliyoshukuru Lady Jaydee mwaka 2016

Lady Jaydee ameitaja talaka yake kutoka kwa aliyekuwa mume wake, Gardner G Habash, ni miongoni mwa mambo 4 aliyoshukuru zaidi kwa mwaka 2016.
Jide alitumia Instagram kuyataja mambo hayo huku la nne akielezea kwa kuweka picha ya cheti cha ndoa na talaka hiyo kutoka kwa mtangazaji huyo wa Clouds FM.


Kwenye post hiyo pia Jide amezungumzia kwa mara ya kwanza video maarufu ya mwaka huu iliyomuonesha Captain akijigamba kumko*oza staa huyo kwa zaidi ya miaka 10.
“Sitegemei tena kauli za nilikufanyaje sijui miaka kadhaa, au emoji zisizo eleweka. Utoto huooooooo . Mtu aki move on hana haja kufanya utoto wote huo , uki move on hujali chochote,” ameandika Jide.

Hii ni post nzima:
No. 4 (Funga Mwaka) Katika vitu vikubwa ninavyoshukuru 2016
Ni kutoka katika Cheti cha juu na kuingia Cheti cha chini ๐Ÿ™๐Ÿ™
Bila kujali wanafikiria nini ๐Ÿ™‹๐Ÿป๐Ÿ™‹๐Ÿป Nilifanya hivyo kwa manufaa na furaha yangu , maisha yangu na familia yangu.Namshukuru Mungu kwa kunipa nguvu kwani haikuwa kazi rahisi ukizingatia swala la kuogopa watu wata ku judge vipi. Baada ya battle ya nafasi ya takribani miaka miwili ๐Ÿ’ช๐Ÿฝ๐Ÿ’ช๐Ÿฝ๐Ÿ’ช๐Ÿฝ๐Ÿ’ช๐Ÿฝ๐Ÿ’ช๐Ÿฝ Naomba makofi tafadhali ๐Ÿ‘๐Ÿ‘๐Ÿ‘๐Ÿ‘
Sitegemei tena kauli za nilikufanyaje sijui miaka kadhaa, au emoji zisizo eleweka. Utoto huooooooo . Mtu aki move on hana haja kufanya utoto wote huo , uki move on hujali chochote. Kwa neema ya Mungu nawaombea Wote ambao hamja get over situations mbarikiwe mtoke kwenye kuwaza past, Maisha mbona ni matamu tu ukiamua
#KataaKuwaMtumwa
#ChaguaKuwaNaFuraha
#GutsOverFear
#Komando
#MoveOnNigga
๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚
Mambo mengine ni pamoja na:
No. 1
Kiukweli Comeback yangu ya 2016 ilikuwa kubwa sana kuliko watu wengi walivyotegemea Mbali na changamoto ngumu na nyingi nilizowahi kupitia na ninazo endelea kuzipitia kuliko msanii yoyote yule wa kike wala wa kiume Tanzania. Nadiriki kusema bado nimesimama Imara ๐Ÿ’ช๐Ÿฝ๐Ÿ’ช๐Ÿฝ๐Ÿ’ช๐Ÿฝ๐Ÿ’ช๐Ÿฝ๐Ÿ’ช๐Ÿฝ๐Ÿ’ช๐Ÿฝ๐Ÿ’ช๐Ÿฝ๐Ÿ’ช๐Ÿฝ *Kejeli *Dhihaka *Mabezo *Kutengwa, *Story za kusingiziwa ikiwemo kuambiwa nyumba yangu inauzwa sijui inapigwa mnada ๐Ÿ™„๐Ÿ™„๐Ÿ™„๐Ÿ™„๐Ÿ™„ na mengine yote mnayoyajua ni vitu vinavyo vunja moyo sana ๐Ÿ˜ข๐Ÿ˜ข๐Ÿ˜ข๐Ÿ˜ข๐Ÿ˜ข๐Ÿ˜ข Ila Wa Tanzania nina waheshimu sana. Linapokuja swala la kupigania kitu mnachokipenda. Hivi bila nyie si ningekuwa marehemu??? Bila fans JayDee ni nani???? Niwashukuru kwa kunisimamisha. Ninawashukuru kwa kuniamini. Ninawashukuru kwa kunipa nguvu na jeuri. Kuanzia NdiNdiNdi mpk Together Remix *Mliijaza Mlimani City
*Mkajaa Mikoa niliopita Nawaomba muendelee kujaa 2017
Ili kuwadhihirishia wanadamu kuwa Mungu huwa ni mmoja tu ๐Ÿ™๐Ÿ™๐Ÿ™๐Ÿ™๐Ÿ™๐Ÿ™ Happy new year to my fans all around the world ๐ŸŽ‰๐ŸŽˆ๐ŸŽŠ๐ŸŽ‰๐ŸŽˆ๐ŸŽŠ๐ŸŽ‰
Nawapenda hata nikinuna ๐Ÿ’‹๐Ÿ’‹๐Ÿ’‹ Kaeni tayari kwa album ya “WOMAN 2017 “
No 2
Kama nilivyo elezea hapo awali. Mwaka 2015 vitu vingi vilisimama ili nijipange upya ๐Ÿ˜ Na 2016 vitu vingi vilianza kurudi
Ikiwemo kuendelea ku perform na Band yangu “THE BAND ” ambayo niliondoa jina la “MACHOZI BAND” na tulizunguka sehemu nyingi nchini ๐ŸŽผ๐ŸŽค๐ŸŽน๐ŸŽท๐ŸŽป๐ŸŽธ๐ŸŽบ Mwaka 2017 nitarudisha kitu kingine ambacho kimekuwa kikiuliziwa na watu wengi sana kutokana na kutokuwepo hewani kwa takribani mwaka na nusu “DIARY YA LADY JAYDEE”
๐ŸŽฌ๐ŸŽฌ๐ŸŽฌ๐ŸŽฌ๐ŸŽฌ๐ŸŽฌ๐ŸŽฌ๐ŸŽฌ๐ŸŽฌ Itarudi tena kwa mfumo na muonekano wa tofauti na wa mwanzo Ukizingatia maisha yangu pia yamebadilika. Hivyo naomba sponsors kujitokeza kwa wingi pia kwani mambo yatakuwa ni ๐Ÿ”ฅ๐Ÿ”ฅ๐Ÿ”ฅ
Itakuwa ni kuhusu maisha yangu binafsi ya ki muziki ๐ŸŽผ, ki biashara ๐Ÿ’ฐmapenzi ๐Ÿ’‘na kila kinacho nizunguka. Kaeni tayari kwa Msimu mpya wa Diary ya Lady JayDee Yenye production bora zaidi ya jana Diary ya Lady JayDee itapatikana pia kwenye YouTube channel yangu fanya ku subscribe

Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment