Vanessa Mdee na Jux wakitaja kitu kinawachowagombanisha zaidi kwenye uhusiano wao

Couple zote, hata zile ambazo katika macho ya nje huonekana kuwa ni ‘perfect combo’, hugombana.


Na wakati mwingi sana, chanzo cha ugomvi huwa ni vitu vya kawaida na vidogo tu. Jux na Vanessa Mdee licha ya kupendana sana, nao pia hujikuta wakifarakana hapa na pale. Nini hasa kinachowagombanisha kwenye uhusiano wao? Vee Money ametaja kuwa ni simu.
“[Jux] ni mbovu wa simu, amefarakanishwa na simu yake jamaa,” amesema Vanessa kwenye kipindi cha Ngaz Kwa Ngaz cha Salama Jabir. “We are far from each other lakini hata kwenye kujibu message au kupokea simu yaani hana ushirikiano na simu kabisa. Kwahiyo tunagombanaga mara nyingi kuhusiana na communication,” ameongeza.
Kwa upande wake Jux alijitetea kwa kusema, “simu zinaisha chaji,” lakini Vee akampinga, “Hata kama ikiwa, nakuona Instagram.”
Kwa upande wa swali la nani anayempenda zaidi mwenzake, kila mmoja alisema upendo wake upo ‘Juu’ kuliko mwingine.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment