Wastara ataja mambo 5 ambayo hatayasahau katika maisha yakeMsanii wa filamu nchini Wastara Juma ametaja mambo matano ambayo hatakuja kuyasahau katika maisha yake.
Muigizaji huo amekiambia kipindi cha FNL cha EATV, jambo la kwanza ambalo hata kuja kulisahau maishani mwake kifo cha wazazi wake wote wawili na jambo la pili ni ajali ambayo ilimsababishia ulemavu mpaka sasa hivi.
Jambo la tatu ambalo Wastara ameongeza hatalisahau ni kifo cha mumewe Sajuki na jambo jingine ambalo linamuumiza na hatalisahau wakati alipotumia vyombo vya habari kuchangisha fedha kwa ajili ya matibabu ya mumewe Sajuki ambaye baadaye alifariki dunia.
Wastara ameweka wazi jambo la tano ambalo linamuumiza zaidi kichwa ni kitendo cha mashabiki wake kumchukulia tofauti na alivyo kiuhalisia
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment