Waziri Mwigulu Nchemba alivyoguswa na hali ya Chid Benz

Hivi karibuni zilisambaa picha kwenye mitandao ya kijamii zikimuonyesha msanii wa Bongofleva Rashid Makwilo ‘Chid Benz’ akionekana kurudi kwenye dawa za kulevya.

 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba amekutana na kufanya mazungumzo na mama wa Chid Benz, baada ya kuonana na mama yake Chid Benz haya ni maneno aliyoyaandika kwenye ukurasa wake wa Instagram……..
Nimekutana na kufanya mazungumzo na mama wa msanii Rashid Makwilo “Chid Benz” ambaye kwasasa amepatwa na tatizo la Dawa za kulevya. Inasikitisha na haivumiliki kuona nguvu kazi ya Taifa inapotea huku wauzaji wakinufaika kwa pesa haramu.
Ifahamike wazi vita ya serikali dhidi ya magenge, wauzaji na wasambazaji wa madawa ya kulevya imeongezeka hasa katika awamu hii ya tano chini ya Mh.Rais J.P.Magufuli,hivyo anayejihusisha kwa namna yoyote ni vema akaamua kuachana nayo kabla hajakutwa na mkono wa dola.
Mbali ya vyanzo vya taarifa tulivyonavyo, ni wajibu wa kila aliye RAIA MWEMA kutoa taarifa zitakazo saidia kuangamiza biashara haramu ya madawa ya kulevya. Naishukuru familia ya Chid Benz kwa jitihada wanazozifanya kuhakikisha kijana mwenzetu anarejea katika hali yake ya kawaida. Unaweza kuimba,unaweza kufanikiwa, unaweza kutatua matatizo yako bila kutumia madawa ya kulevya.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment

Note: only a member of this blog may post a comment.