Yaliyojiri Weekend ,Kenya yafanya Vyema Miss Universe 2017, Uamuzi wa kujiuzulu kwa Mkuu wa Wilaya ya Uyui Tabora,EFM yazoa tuzo nne kwenye Tanzania Leadership AwardsShindano la 65 la kumtafuta Miss Universe limemalizika huko Ufilipino ambapo Mshindi ametangazwa kwamba ni Iris Mittenaere wa Ufaransa huku nafasi ya pili ikichukuliwa na Haiti kupitia kwa Raquel Pelissier na namba 3 akiwa ni Andrea Tovar wa Colombia.

Miss Universe 2017 Top 6 imetangazwa, Mshiriki pekee wa Afrika kwenye list ni #MissUniverseKENYA #MissKenya #MaryEstherWere #Top6


Tanzania iliwakilishwa na Jihan Dimack Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amemjibu Mkuu wa Wilaya ya Uyui mkoani Tabora aliyeomba kujiuzulu wadhifa huo.


Katika majibu yake Rais Magufuli ameridhia uamuzi huo na kwamba uteuzi wa mtu mwingine atakayejaza nafasi hiyo utafanyika baadaye.
Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu Gerson Msigwa imesema
“Ombi la Bw. Gabriel Simon Mnyele aliyeomba kujiuzulu wadhifa wake wa Mkuu wa Wilaya ya Uyui Mkoani Tabora limekubaliwana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli. Nafasi ya Mkuu wa Wilaya ya Uyui Mkoani Tabora itajazwa baadaye.”
Taarifa za kujiuzulu kwa mkuu huyo wa wilaya zilianza kusambaa jana zikidai kuwa aliaga katika Kamati ya Madiwani wa CCM na kamati ya siasa ya wilaya, pamoja na kutoa taarifa kwa Mwenyekiti wa Halmashauri kuwa ameamua kuchia ngazi, bila kueleza sababu za uamuzi huo.
Hata hivyo baadaye kulitokea utata baada ya kusambaa kwa taarifa za yeye kukanusha kufanya uamuzi huo, lakini sasa ni dhahiri kuwa Bw. Gabriel Simon Mnyele siyo mkuu wa wilaya hiyo tena.
Bdozen alikutana na JaneGoodall huyu mwanamama ni mtu maarufu ambaye anafanya kazi nzuri ya utafiti wa sokwe na Hamisi Mandi ali share picha hii kwa insta na caption hii 

She is a highly respected member of the world scientific community and is a staunch advocate of ecological preservation! 
Kama humfahamu huyu mama, anaitwa JaneGoodall, Moja kati ya watafiti wanasayansi wenye heshima yao Duniani!! Sifa kubwa amepata kwenye study za chimpanzees (sokwe) ambao hua anaishi nao sometimes kujifunza tabia zao!!
EFM imejizolea tuzo nne kwenye  Tanzania Leadership Awards, Vipengele ilivyoshinda ni pamoja na redio bora ya mwaka, kampuni bora kwa ubunifu, kampuni inayokuwa kwa kasi pamoja na tuzo ya mwandishi bora ya mwaka ambayo imekwenda kwa mtangazaji wa kipindi cha Uhondo katika redio hiyo Dina MariosJan 29 Mwanadiplomasia Ombeni Yohana Sefue aliteuliwa na kuwa Mtanzania wa kwanza kuwepo kwenye jopo la watu mashuhuri kwenye mpango wa bara la Afrika wa kujitathmini kiutawala bora. (APRM)
Katibu mtendaji wa APRM Tanzania Rehema Twalib anayehudhuria mkutano wa umoja wa Afrika Addis Ababa amesema Katibu kiongozi huyu wa zamani Ikulu ya Tanzania ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 62, ameidhinishwa kwenye kikao cha juu cha Wakuu wa nchi za umoja wa Afrika ambao ni Wanachama wa APRM.
Jopo la watu mashuhuri ni chombo cha juu cha kuwashauri  wakuu wa nchi wanachama wa APRM kwenye uendeshaji wa huo mpango kwenye kusimamia mpango mzima wa kujitathmini ambapo Wajumbe wa jopo hilo hudumu kwa miaka minne.
Mchakato wa kuteua wajumbe hao huanzia kwenye kupendekezwa na nchi zao na baada ya mlolongo mrefu ambao una ushindani, majina ya waliokidhi vigezo hupelekwa mezani na kuidhinishwa na kikao cha juu cha APRM.
Kwenye mkutano huo Addis Ababa Mwenyekiti wa Wakuu wa nchi APRM Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya aliwapongeza wajumbe wa jopo hilo na kuwataka washiriki vyema kuifanya APRM kuwa chombo chenye thamani Afrika kama Waasisi wake kina Benjamin MkapaObasanjo na Thabo Mbeki walivyotarajia.

Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment