Duniani kuna mambo::Mtoto wa mfalme alivyowalipia ndege aina ya KIPANGA nauli na kuwapandisha Ndege ya abiria

Kiswahili kizuri cha Falcons ni KIPANGA ila halijulikani sana hili la kiswahili.


Kutoka Saudi Arabia leo mtoto wa mfalme wa nchi hiyo Prince Mohammed Bin Salmanambaye pia ni waziri wa ulinzi ndio anamiliki vichwa vya habari.
Uamuzi wake wa kusafiri na Ndege jamii ya kipanga wapatao 80 kwenye ndege ya abiria ndio umekua gumzo ambapo ndege hiyo inatajwa kuwa ya shirika la Qatar Aiways. 
Kikawaida ni jambo gumu kuwasafirisha ndege ndani ya ndege tena wanaofikia 80 labda tu uwe mtoto wa mfalmee kama ambavyo Prince Mohamed amefanya hivi karibuni baada ya kuamua kuwalipia nauli mwewe 80 kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 100 ili kupata siti za ndege hao.


Kwa mujibu wa rafiki wa karibu wa Prince Mohamed inaelezwa kuwa ni kweli kitu hicho kimefanyika na waliwafunga mabawa Mwewe wote ili wasiruke wakati ndege ikiwa safarini

Inaelezwa kuwa sio jambo geni kusafirisha wanyama au ndege lakini hawatakiwi kuzidi 6 tu, sasa ili upate ruhusa ya kusafirisha idadi kubwa lazima ulipe fedha nyingi au uwe na kibali maalumu cha viongozi wakuu wa nchi kama ilivyokuwa kwa mtoto wa mfalme.
Hili naona la kawaida Tanzania yetu watu wanasafirisha Twiga mchezoo.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment