Ester Bulaya: Mdogo wangu anayenifuata ni mwathirika wa unga, naujua uchungu wake

Mbunge wa Bunda Mjini Ester Bulaya, amedai kuwa mdogo wake pia ni mwathirika wa dawa za kulevya ambaye kwa sasa anatumia dawa ya methadone kwenye hospitali ya Mwananyamala.


Akiongea bungeni Jumatatu hii, Mheshimiwa Bulaya alisema kutokana na ukweli huo, anaelewa vyema uchungu wa madhara yatokanayo na matumizi ya dawa hizo na kwamba vita lazima iendelee, japo kwa njia inayofaa.
“Mimi mwenyewe mdogo wangu anayenifuata yupo Mwananyamala anakunywa dawa pale methadone, kwahiyo ninachokisema nina uchungu nacho na nimefikifanyia utafiti wa kina na nilileta maelezo binafsi katika bunge hili tukufu,” alisema Bulaya.
Mbunge huyo alimshauri Mkuu wa mkoa wa Dar, Paul Makonda kuwa watu wanaotumiwa madawa ya kulevya wanatakiwa kusaidiwa kwa kupelekwa hospitali na kwamba anatakiwa kuwahoji watu waliofungwa magerezani kwa kujihusisha na biashara hiyo ili kuwataja wenzao.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment