Jiandae kwa concert kubwa ya uzinduzi wa album mpya ya Lady Jaydee ‘Woman’ mwezi ujao


Kama wewe ni shabiki wa Lady Jaydee, hii ni habari njema kwako.
Muimbaji huyo mkongwe anatarajia kufanya concert kubwa kwaajili ya uzinduzi wa album yake mpya Woman. Jaydee ameitoa habari hiyo kupitia kipindi cha The Playlist cha Times FM.

“Natarajia kufanya concert kubwa kwaajili ya launch ya album ya Woman ambayo itakuwa ni mwishoni mwa mwezi March,” alisema.

“Na album yenye nategemea kuitoa mwezi ujao kwasababu siwezi tena kusubiri zaidi. Ilikuwa itoke mwaka jana mwishoni lakini kutokana na mipangilio kuwa haijakamilika, tukaisogeza mbele ili tufanye kitu kizuri zaidi kwa watu. Kwahiyo wajiandae kwa concert kubwa,” aliongeza.

Jide ameongeza kuwa kabla ya album haijatoka, ataachia nyimbo mbili alizowashirikisha wasanii kutoka nchi za Afrika.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment