Linah auzungumzia ujauzito wake, mpenzi wake anayeishi naye na mengine

Msanii wa muziki Linah Sanga amefunguka na kuzungumza hukusu ujauzito wake baaada ya kukaa kimya kwa muda mrefu bila kulizungumzia suala hilo.


Akiongea na Bongo5 wiki hii akiwa pamoja na mpenzi wake huyo ambaye pia ni bosi wake, Linah alidai anafuraha kuwa mjamzito kwa kuwa ni kitu ambacho alikuwa nakitamani kwa muda mrefu.
“Ninafuraha kubwa kwa sababu ni kitu ambacho kama mwanamke nilikuwa nakitamani siku zote kwamba na mimi nije niitwe mama, nafuraha nimepata mtu sahihi wa kuzaa naye na kuamua kulea naye watoto,”alisema Linah huku akiwa mwenye furaha.
Kwa upande wa mpenzi wake ambaye pia ni mkurugenzi wa kampuni Drops Up Entertainment ambayo inamsimamia Linah, alisema wao kama kampuni wamejipanga kuhakikisha Linah wanamsfikisha mbali zaidi.
“Tuna mipango mikubwa kwa Linah kwa sababu kila kitu ambacho tulikuwa tunafanya kwa mpango tuliangalia sasa hivi yupo kwenye hali fulani, kwa hiyo management imejipanga kuhakikisha Linah anafika sehemu fulani. Pia kwa mwaka huu Linah time table yake imetimia, ana audio zakutosha pamoja na video za mwaka mzima,”

Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment