Mbowe hajakamatwa, ameenda mwenyewe Polisi Na Freeman Mbowe Aaachiwa na polisi usiku wa manane

Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe ameenda mwenyewe kwenye kituo cha Polisi, Central jijini Dar es Salaam si kwa kukamatwa, taarifa ya cha hicho imesema.
Taarifa hiyo inakinzana na zile zilizosambaa mchana kuwa Mbowe alikamatwa na polisi maeneo ya Mikocheni ambako alienda kujificha ili asikamatwe.
Taarifa ya katibu wa chama hicho mkoa wa Dar es Salaam, H Kilewo imesema

Waheshimiwa Viongozi na Wanachama wa Chadema Dar es salaam, Siku ya leo Mwenyekiti wa Chama Mhe.Freeman Mbowe akiwa Kwenye Mkoa wetu wa Dar es salaam, Ameamua kwenda Central baada ya kuwepo na Taarifa nyingi kwenye vyombo vya habari na Mitandao ya kijamii kuwa anahitajika nao. Taarifa za kusema ya kwamba jeshi limemkamata na kumpeleka Central ni taarifa za uongo ambazo hatujui zinataka kulenga kitu gani…Taarifa sahihi ni Kwamba Mhe.Freeman Mbowe ameamua kwenda baada ya taarifa kuzagaa kuwa anatafutwa
Siku ya Jumamosi Kamanda wa polisi kanda maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro alimpa kiongozi huyo muda wa saa 48 za kujisalimisha vinginevyo watamtafuta kwa njia wanazozijua wao.
Mbowe aliitwa polisi kwaajili ya mahojiano kutokana na tuhuma za kujihusisha na biashara ya madawa ya kulevya pamoja na kulisababishia usumbufu na gharama jeshi la polisi.
BUT JANA  USIKU WA MAANANE KUAMKIA LEO WAMUACHIA HURU 
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe ameachiwa saa saba na robo usiku wa kuamkia leo baada ya kuhojiwa na Jeshi la Polisi.
Mbowe alikamatwa Jumatatu hii jioni wakati akienda kujisalimisha polisi na kupekuliwa nyumbani kwake kabla ya kuhojiwa hadi alipoachiwa usiku. Ofisa habari wa chama hicho, Tumaini Makene ameithibitishia Mwananchi Digital taarifa za kuachiwa mwanasiasa huyo kuwa ni za kweli.
Hata hivyo, taarifa iliyosambazwa na Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Salum Mwalimu kupitia mitandao ya kijamii imesema kuwa chama hicho kitatoa taarifa zaidi juu ya tukio hilo leo.
“Tunawashukuru wote kwa sala, maombi na subira na hivyo kuhitimisha salama saa kumi za mwenyekiti wetu kuwa chini ya Jeshi la Polisi katika Kituo Kikuu cha Polisi, Dar es Salaam,” Mwalimu amesema.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment