MHESHIMIWA CHABAKA KILUMANGA BALOZI WA TANZANIA VISIWANI KOMORO ASHITUKIZWA KWA KUTUNUKIWA MEDANI YA HALI YA JUU YA HESHIMA NA MHE. AZALI ASSOUMANI RAIS WA MUUNGANO WA VISIWA VYA KOMORO LEO HII TAREHE 16 FEB 2017

 Balozi wa Tanzania ndani ya Muungano wa Visiwa vya Komoro Mhe. Chabaka Kilumanga ASHITUKIZWA kwa Kutunukiwa Nishani ya Juu (Highest Civilian Honor) na Rais wa nchi hiyo Mhe. Azali Assoumani. Mhe. Balozi ambaye aliongozana na Mkewe Bi Irene J. M. Kilumanga walishiriki katika hafla hiyo iliyofanyika Bait Salam, Ikulu ya Komoro leo tarehe 16, Feb, 2017. Wageni waalikwa walioshuhudia  hafla hiyo ni pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje wa Komoro Mhe. Baccar Dossar na Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Komoro Mhe. Yousef Mohamed Yousef


.

> Hafla hiyo ilifanyika ikiwa ni sehemu ya sherehe ya kumuaga Balozi huyo ambaye atastaafu na kumaliza muda wake wa kazi Visiwani Komoro  ifikapo tarehe 17 Machi, 2017...
> Mhe. Balozi Chabaka Kilumanga anakuwa ndio Balozi wa mwanzo kutunukiwa medani hiyo miongoni mwa mabalozi wenzake wanao tumikia nchi zao Visiwani Komoro. Wakati akimtunuku medani hiyo, Mhe. Rais Azali alieleza kutambua mchango mkubwa aliofanya Mhe. Balozi huyo katika kudumisha uhusiano mzuri uliopo baina ya Tanzania na Komoro, pamoja na kumpongeza kwa utumishi uliotukuka.
>
> Kwa upande wake Mhe. Balozi alieleza kufarijika sana kwa na kupata mshtuko mkubwa kwa KUSHITUKIZWA kutunukiwa Nishahi hiyo ambayo imekuwa ni heshma kubwa kwake. Katika risala yake Mhe. Balozi Chabaka Kilumanga alieleza kwamba kutunukiwa Nishani hii ya kiwango cha juu ni HESHIMA KUBWA KWAKE na NCHI YAKE TANZANIA, na alipongeza juhudi za Serikali ya Mhe Azali kwa hatua inazochukua katika kuleta maendeleo kwa wananchi wa Komoro. Aidha alipendekeza kwa Serikali hiyo kuanza kufanya taratibu za kujiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kupanua wigo wa ushirikiano baina ya Tanzania na Komoro.
>
> Kutunukiwa kwa medani hiyo kulikuwa ni kwa kushtukiza kwani Mhe. Balozi hakutarajia kabisa kutunukiwa nishani hiyo ambayo kwa kawaida hupewa raia wa Komoro ambao wametoa mchango mkubwa katika maendeleo ya Taifa lao. Hivyo hii imekuwa ni heshima kubwa sio tu kwa Mhe. Balozi bali pia kwa Taifa la Tanzania kwa ujumla.
>
> Wakati wakiagana na Mhe. Rais, Mhe. Balozi na Mkewe Bi Irene J. M. Kilumanga walieleza kuwa kamwe hawatasahau upole na ukarimu wa Wakomoro na kwamba Komoro itaendelea kuwa mioyoni mwao daima.

Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment