Msg ya kwanza ya Shamsa Ford kwa Mumewe toka aende Polisi kwa sakata la dawa za kulevya

Mwigizaji Shamsa Ford ambaye ni mke wa Mfanyabiashara Chidi Mapenzi aliyeitwa Polisi kwa tuhuma za kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya, ameandika yafuatayo ikiwa ni mara ya kwanza toka aitwe Polisi kuhojiwa.

Shamsa amepost ujumbe huu kupitia Instagram “nilipoolewa nilijua ipo siku nitapitia hivi vitu huzuni,furaha, maudhi, kudharauliwa, kuchekwa na nk.ila pamoja na yote hayo haitabadilisha mapenzi yangu kwa mume wangu kipenzi”
Nina amini kuwa wewe ni mume aliyenipa Mungu na wala Mungu hakutukutanisha kwa bahati mbaya.Dunia nzima ikuzomee na kuamini kile wanachoamini lakini jua una mke anayekupenda kwa dhati
Ninakujua, ninakuamini na kukupenda sana ndomaana niliolewa na wewe kwasababu nilijua utakuwa baba bora kwa mwanangu kama ambavyo ulivyo sasa..Nina amini Mungu anapotaka kukupeleka sehemu anayoitaka yeye lazima akupitishe kwenye mitihani”
Hii ni mitihani ya Mwenyezi Mungu na nina imani inshaallah yatapita..Nakupenda sana mume Wangu kipenzi Rashidi..

Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment