Mzee wa Upako azungumzia tetesi za kula ulabu

Mchungaji Anthony Lusekelo maarufu kama ‘mzee wa upako’ amefunguka kuhusu tuhuma za yeye kunywa pombe, na kuweka wazi kuwa hanywi pombe bali anakunywa ‘wine’ isiyo na kilevi, huku akisema kuwa amewasamehe waandishi aliwowatabirian kifo.


Amefunguka hayo kwenye kipindi cha KIKAANGONI cha EATV, na kuweka wazi kuwa wanaomtuhumu kuwa yeye anakunywa pombe wanapaswa kutoa ushahidi juu ya tuhuma hizo, na kwamba unywaji pombe unaweza kuwa dhambi ama usiwe dhambi kulingana na imani na dini ya mtu. “Hao wanaotuhumu kuwa nakunywa pombe, waeleze ni pombe gani nakunywa, nilikuwa nakunywa wapi na aliyeniona ni nani, kuna sehemu nyingine pombe siyo dhambi, dini nyingine mpaka kanisani kuna bar.”
Alipoulizwa Je, kunywa bia kiasi bila kulewa ni dhambi au siyo dhambi? alijibu kuwa “Inategemea na makanisa, kuna mengine hata kunywa soda ni dhambi. Dhambi ni makubaliano yenu kwenye dini yenu. Biblia inasema kula kitu chochote hata chakula kama ukila kupitiliza ni dhambi, hata unywaji wa pombe ukinywa ukapitiliza ni dhambi. Biblia haijaandika moja kwa moja kwamba msinywe pombe, imesema msilewe kwa kuwa ndani ya ulevi kuna ufisadi, cha msingi mbadilishe ulevi wenu uwe ni roho mtakatifu”
Aidha mzee wa upako alipoulizwa kuhusiana na ahadi yake hiyo ya kuwatabiria vifo waandishi walioandika habari iliyohusisha kurushiana maneno na jirani zake ambapo baada ya hapo vyombo vya habari hasa magazeti yaliripoti tukio hilo kwa namna ambayo Mzee wa Upako hakuipenda, na hata kufikia hatua ya kuwatabiria kifo waandishi walioandika habari hiyo, amesema:
“Tulisema hatuwezi kutumia nguvu kubwa sana kuwaombea watu kifo, kwa sababu sisi ni wanadamu, na wanadamu tuna mapungufu kwahiyo nikaona ni bora kumuachia Mungu. Uwezo huo wa kuwaombea watu wakafa, mimi ninao, lakini nikaona inasaidia nini mtu kumuombea mabaya, kwahiyo nikaamua kusamehe.”

Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment