Nakuja na orodha ya watuhumiwa ushoga wanaojiuza mtandaoni- Kigwangalla

Ushoga ni suala ambalo limekuwa likilalamikiwa mitandaoni na baadhi ya watu ambapo watu wengi wanaoneshwa kukerwa na mapenzi hayo ya jinsia moja huku serikali ikioneshwa kuanza kuweka nguvu kuyapinga vikali.

Naibu Waziri wa Afya, Ustawi wa jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk. Hamis Kigwangalla, ameandika ujumbe mwingine Twitter akitangaza vita yake dhidi ya watu wanaojinadi kufanya mambo hayo.
“Uchunguzi dhidi ya watuhumiwa wa ushoga unaendelea. Watakamatwa kimya kimya! Serikali ina mkono mrefu. Wakipatikana watatusaidia wenza wao.Kuna watu wanadhani vita dhidi ya ushoga ni ya mzaha, ni vita kubwa na tutaishinda. Mtandao ni mrefu na nitaendesha operation kamata kamata,” aliandika.
“Namalizia ziara jimboni. Nikirudi Dar, kabla ya kuhamia rasmi Dodoma, nitaweka wazi orodha ya watuhumiwa wa ushoga wanaojiuza mitandaoni. Kuna nchi marafiki zetu zinafanya jitihada za kupenyeza ushoga Tanzania na kudai ni haki ya binadamu kuchagua ampendaye, sisi tunasema NO!.”
“Ushoga hauna addiction wala siyo wa kuzaliwa nao, wanaofanya hivyo wanajiendekeza tu! Ushoga siyo biological. Mashoga wote waache mara moja,” ameonya.
Hivi karibuni waziri huyo alitaja baadhi ya watu wanaotuhumiwa kuwa ni mashoga akitaka wajisalimishe katika vyombo vya sheria kabla ya kutafutwa.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment