Nataka harusi yangu na Diamond iwe kubwa na ya gharama kuwahi kutokea Afrika Mashariki – Zari

Zari The Bosslady amedai kuwa anataka harusi yake na Diamond Platnumz iwe kubwa na yenye gharama kuwahi kufanyika Afrika Mashariki


Hata hivyo, itafanyika baada ya kuwa wamefanya mambo ya muhimu zaidi ikiwemo kujijenga zaidi walivyo sasa. Akizungumza kwenye kipindi cha Leo Tena cha Clouds FM Alhamis hii, Zari amedai kuwa suala la kufunga ndoa sio kitu kinachowapa pressure.
Amedai kuwa hawajawahi kukaa chini na kuwa na majadiliano ya kina kuhusu ndoa, licha ya hadi sasa kuwa na watoto wawili, Tiffah na Nillan. Staa huyo wa Uganda amedai kuwa moja ya mambo ambayo wanataka kufanya ni kuhakikisha kwanza wanawajengea watoto wao apartments zao zitakazowasaidia katika maisha yao hata kama wazazi wao wasipokuwepo.
Hata hivyo Zari amedai kuwa mwezi March mwaka huu Diamond ataenda rasmi kujitambulisha kwa baba yake na kuhalalisha uhusiano wao pamoja na kuomba mkono wa ndoa.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment