Rais Magufuli akerwa na kitendo cha Manji na Gwajima kwenda na mashabiki wao Polisi

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Dar es Salaam, Dkt John Pombe Magufuli amechukizwa na kitendo cha watu kwenda Kituo Kikuu Polisi (Central) na kuanza kuosha gari la mtuhumiwa huku wengine wakienda na kwaya katika eneo hilo.
Rais Magufuli ameyasema hayo wakati wa kuwaapisha maafisa mbalimbali huku akiwaagiza kuchapa kazi bila kumuogopa mtu yeyote. Tukio hilo lilitokea Alhamisi iliyopita wakati mwenyekiti wa Klabu ya Yanga, Yusuf Manji alipokwenda kuripoti polisi na baadhi ya mashabiki wake kuosha gari lake lililokuwa limeegeshwa katika kituo hicho.

Wengine wanaoaminika kuwa ni wanakwaya wa Kanisa la Ufufuo na uzima linaloongozwa Askofu Josephat Gwajima walifika eneo hilo wakati kiongozi wao alipokwenda kuhojiwa huku wakiimba nyimbo mbalimbali.
“Sitaki kuona tena wananchi wanajazana kituo cha polisi watuhumiwa wanapohojiwa. Lazima tujenge nidhamu, mbona hawakwenda Lugalo kwa CDF (Mkuu wa Majeshi) kuimba kwaya?” amesema Rais Magufuli huku akimuagiza Kamishna wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro kuwa mkali.

Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment