Ridhawani Kikwete aitaka serikali kuwachukulia hatua kali wafanyabiashara wa dawa za kulevya

Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete, amefunguka kuhusu sakata la dawa za kulevya na kuipongeza serikali hususani Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kwa kuanzisha vita hiyo na kutaka wahusika wachukuliwe hatua.


Ridhiwani Kikwete
Akiongea Jumatano hii katika kipindi East Africa Breakfast cha EA Radio, Ridhiwani ameishauri serikali kuifikisha mwisho vita hiyo, ili kulimaliza kabisa tatizo hilo kwa kuwa limepoteza vijana wengi wenye uwezo mkubwa na mchango katika taifa.
“Kwanza nataka kusema hii vita ni jambo jema sana, unajua jamii yetu hasa hasa kama hayajakukuta kwenye familia yako huwezi kuelewa ukubwa wa tatizo na madhara yake,” alisema Ridhiwani. “Kwa mfano mimi katika maeneo ambayo naishi, kuna watu ambao walikuwa katika umri wetu tumewapoteza, kwa mmfano vijana kama akina Langa wale, tumejaribu kuwasaidia mpaka ikaonekana hakuna njia ambayo unaweza ukawasaidia tena, sisi kwetu tunaumia kwa kuona hawa vijana walikuwa na future nzuri sana.
“Kwahiyo kwangu mimi hii vita hatutakiwi kushindwa, na kwangu mimi kama kiongozi kijana nipo pamoja na serikali katika kuhakikisha jambo hili linafika mwisho. Hata kama hatutalifikisha mwisho kwa maana ya mwisho, kwa sababu vita hii ni vita pana, wewe mwenyewe unaona Marekani imenza vita hii toka miaka 80 lakini mpaka leo wanaendelea kupambana,”.
Aliongeza, “Kwa hiyo hii ni vita ambayo inatakiwa kuwa katika ajenda ya nchi, ajenda ya Taifa hili, kwa mfano sasa hivi imeundwa hii timu ya Bwana Sianga ambaye kwangu mimi ni mtu ambaye nikisoma kwenye CV yake ni mtu mzuri sana na makini, ni mmoja kati ya Watanzania wachache ambao walipata nafasi ya kwenda kusomea madawa ya kulevya. Lakini la msingi zaidi ambalo tunatakiwa kulifanya hasa hasa Watanzania nikuwapa ushirikiano mkubwa sana, ni watu professional, watachunguza watu namshukuru Mkuu wa mkoa siku ile amemkabidhi majina yale, tunaamini kabisa watachunguza watu na wale ambao watakutwa na hatia lazima washughulikiwe, washughulikiwe ili jamii yetu iwe safe,”
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment