Sirro: Tulipata taarifa huenda Masogange ni kati ya wauzaji au wasafirishaji wa unga (Video)


Kamanda wa Polisi kanda maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro amedai kuwa sababu ya kumshika mrembo maarufu wa video za muziki nchini, Agnes ‘Masogange’ Gerald ni kupata taarifa kuwa huenda akawa mmoja wa wauzaji, watumiaji ama wasafirishaji wa dawa za kulevya.

“Kwahiyo tumemhoji, tumemsachi na tumempeleka kwa mkemia wa serikali,” Sirro amewaambia waandishi wa habari Alhamis hii iliyopita 

“Kwahiyo tunasubiri tupate majibu ili tuweze kuchukua hatua. Hatua yenye inaweza kuwa ni kumpeleka mahakamani kwa kosa lake ambalo litakuwa limebainika.. tumeona amekuwa na tabia ambazo sio nzuri au itakavyokuwa vinginevyo kutokana na hatua ambayo kutokana na ushahidi tutakaokuwa tumeupata,” ameongeza.
Masogange alikamatwa February 14, 2017 na kufanya idadi ya watu waliokamatwa hadi sasa kufikia 349

Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment