Tunda Man adai amepokea simu nyingi baada ya jina Tunda kutajwa kwenye list mpya ya Makonda

Msanii wa muziki Tunda Man amedai jana alipokea simu nyingi baada ya Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda kutangaza list mpya ya majina ya watu wanaotuhumiwa kujihusisha na biashara ya Madawa ya kulevya ilikiwemo jina la Tunda ambaye ni video queen.Baadhi ya waandishi kwenye mitandao ya kijamii waliandika jina Tunda bila kutolea ufafanuzi ni Tunda gani, hali ambayo iliwafanya wasiohusika kupigiwa simu nyingi akiwemo msanii wa muziki Tunda Man.
Tunda Man amedai wengi ambao ulikuwa wanampigia simu walitaka kujua kama kweli ni yeye ndiye aliyetajwa au ni Tunda mwingine.
“Jaman Tunda alietajwa na Mh Paul Makonda ni huyu sio mie maaana simu zimekuwa nyingi @soudybrown na wewe hujui au umeamua tu kunipigia,” aliandika Tunda Man Instagram huku akiwa amempost dada huyo.
Pia kwenye list hiyo mpya alitajwa mwanadada Vanessa Mdee ambaye pia anatakiwa kuripoti makao makuu polisi Jumatatu
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment

Note: only a member of this blog may post a comment.