Wanaume wenye sura mbaya huamsha zaidi hisia zangu za kimapenzi – Irene Uwoya

Hujiamini kutupa karata yako kwa muigizaji mrembo Irene Uwoya sababu unahisi huna sura nzuri na ya kuvutia? Basi unaichezea bahati yako sababu unaweza kuwa na nafasi kubwa zaidi

Kwa mujibu wa Irene, wanaume wenye sura mbaya ndio ambao huamsha zaidi hisia zake za kimapenzi! Strange, lakini ndio ukweli wake. Muigizaji huyo ambaye ameandaa event maalum kwaajili ya Valentine’s Day aliyoipa jina, ‘Irene Uwoya Valentine’s Special Night, ameahidi kueleza baadhi ya mambo ambayo watu hawafahamu kuhusu yeye katika sekta ya malavidavi.
“Kitu ambacho hamkijui kuhusu mimi ni kuwa sijawahi kuvutiwa na wanaume wenye mionekano mizuri, sielewi ni kwanini lakini wanaume wenye sura mbaya huwa wanaamsha hisia zangu za KIMAPENZI,” ameandika Uwoya.
Wanaume wenye sura nzuri, poleni!
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment