Wema Sepetu athibitisha kutolipwa na CCM fedha zake za kampeni 2015


Malkia wa filamu nchini Wema sepetu amethibitisha kuwa japo amekihama Chama cha Mapinduzi lakini bado alikuwa anadai madeni yake yaliyotokana na kampeni za uchaguzi mkuu alizofanya mwaka 2015 akiwa na wasanii wengineAkiongea mbele ya waandishi wa habari pamoja na baadhi ya wanachama wa Chadema leo hii, Wema amesema walikuwa wanakidai chama hicho yeye na wasanii wenzake wengine lakini wamekuwa wakiambia madeni hayo wakamdai Rais mstaafu wa awamu ya nne Jakaya Kikwete.
“Kuna madeni kweli ambayo wasanii wenzangu wanadai nikiwemo mimi lakini cham kama chama kinajua chenyewe, nikianza kuongelea madeni nitakuwa kama nakumbuka shuka asubuhi,” amesema Wema.
“Madeni yapo kama hilo ndio swali na wasanii wenzangu wengi wanakidai Chama cha Mapinduzi lakini sasa tumekuwa tunaambiwa tumfuate tumfuate JK. Tumfuate JK tukamdai na maneno mengine mengi ambazo ni fununu tumekuwa tunasikia,” ameongeza.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment