Wema Sepetu nje kwa dhamana hadi Feb 28, asomewa mashtaka matatu

Miss Tanzania 2006 na muigizaji wa filamu, Wema Sepetu, Alhamis hii alipandishwa kizimbani kwenye mahamaka ya Kisutu jijini Dar es Salaam.Mrembo huyo amesomewa mashtaka matatu. Ameachiwa kwa dhamana hadi February 28 kesi yake itakaposomwa tena. Wema alikuwa anaendelea kushikiliwa na polisi jijini Dar es Salaam kwa tuhuma za dawa za kulevya ambapo awali alinyimwa dhamana.
Kamanda wa Polisi wa Kanda maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro alisema jeshi lake bado lilimshikilia Wema na wenzake saba ambao walikamatwa na vielelezo na kuwa jalada lao lilipelekwa kwa wakili wa serikali alipitie ili aone ushahidi uliopo pamoja na kupata majibu kutoka kwa mkemia mkuu wa selikali kubaini kama kweli ni mtuamiji wa madawa ya kulevya.
Miongoni mwa mashtaka yanayomkali Wema Sepetu ni kukutwa na msokoto wa bangi nyumbani kwake.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment