Baby J aangusha party ya nguvu kusherekea birthday yake na kuzindua Baby J Foundation (Picha)

Msanii wa muziki mwenye kipaji cha kuimba cha hali ya juu kutoka Visiwani Zanzibar, Baby J Jumamosi hii amesherekea birthday yake kwa kuzindua Foundation yake itayokuwa inasaidia wasanii wachanga kwa kuwaonyesha njia.
Sherehe hiyo iliyofanyika katika Hotel ya Muruhubi Resort Mjini Magharibi, Zanzibar ilihudhuriwa na wadau mbalimbali wa muziki kutoka Zanzibar na Tanzania bara huku mgeni rasmi akiwa Mkuu wa mkoa wa Mjini Magharibi, Mh Yusuph Mohammed.
Akizungumza na waandishi katika uzinduzi huyo, Baby J amedai nia yake ni kuwakomboa wasanii wachanga wa Zanzibar ambao wamekata tamaa kuhumu muziki wao.
“Leo ni siku yangu ya kuzaliwa lakini pia nimeona sio siku ya kusherekea na kula keki tu ni siku ambayo naweza kuitumia kufanya kitu ambacho kinaweza kukumbukwa na Wanazanzibar ndio maaana nikaamua kuanzisha Foundation ambayo itakuwa inasaidia wasanii wachanga kufika sehemu nzuri ambayo itawafanya wategemee muziki kuendesha maisha yao,”
Aliongeza, “Kwa hiyo nashukuru kwa huu mwanzo ni mzuri kwa sababu tumekutuna na Mkuu wa mkoa na kumweleza changamoto zetu, sio tu kusaidia Foundation lakini pia kuwasaidia wasanii wa muziki ambao walikuwa wanashindwa kutoboa wenyewe kutokana na hali ya muziki ilivyo,”
Pia muimbaji huyo amewataka mashabiki wa muziki wake kukaa mkao wa kula kwajili ya ujio wa kazi zake mpya ambazo zitaanza kutoka hivi karibuni.
Kwa upande wa Mkuu wa mkoa wa Mjini Magharibi, Mh Yusuph Mohammed ameahidi kushirikiana na mamlaka mbalimbali za muziki Zanzibar ili kuhakikisha muziki wa Zanzibar unakuwa juu pamoja na kulinda kazi za wasanii.
Mkuu wa huyo alisema tayari ameshafanya vikao mbalimbali na wasanii wa muziki pamoja wadau mbalimbali
kwajili ya kuangaliwa namna ya kuwasaidia wasanii.Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment