BASATA yaufungia wimbo ‘Wapo’ wa Nay wa Mitego (Video)

Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) limeufungia wimbo ‘Wapo’ wa rapa Nay wa Mitego kwa madai wimbo huyo hauna maadili.
Rapa huyo ana siku ya pili anashikiliwa na jeshi la polisi kutokana na wimbo huo.

Akizungumza na waandishi wa habari Jumatatu hii Katibu Mkuu wa Baraza la Sanaa Taifa, Godfrey Mngereza amesema ni marufuku wimbo huo kupigwa sehemu yoyote kutokana na maudhui mabaya ya wimbo huo.

“Tunatangaza rasmi kuufungia wimbo mpya wa Nay wa Mitego, huu wimbo hauna maadili, marufuku hii siyo kwa redio pekee au runinga, kwenye mitandao ya kijamii, kuna mamlaka ambazo zinasimamia hilo kwa hiyo wananchi wanatakiwa kuwa Maliki,”

Alisema kwa sasa baraza hilo litamwita rappa huyu kwajili ya mahojiano na kutoa adhabu nyingine kutokana na huyo kurudia kosa hilo mara kwa mara.

Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment