CCM yatangaza majina ya wagombea ubunge wa Bunge la Afrika Mashariki

Chama cha Mapinduzi (CCM) kupitia Katibu wa Itikadi na Uenezi, Humphrey Polepole kimetaja majina ya wanachama wake 12 walioteuliwa kugombea ubunge wa bunge la Afrika Mashariki, mkutano unatarajia kufanyika kwenye mkutano wa bunge ujao.

Akisoma majina hayo kwa wanahabari,Polepole amesema kuwa wamewateua wanachama hao zaidi ya 400 waliokuwa wamechukua fomu kugombea.
Aidha Chama hicho kimesema kuwa miongoni mwa wabunge 9 watakaokwenda Bunge la Afrika Mashariki kuiwakilisha Tanzania, 6 watatoka CCM. Kufuatia idadi hiyo CCM imesema kuwa itatoa wabunge watatu wa kiume na watatu wa kike ambapo miongoni mwao wanne watatokea Tanzania Bara na wawili watatokea Tanzania Visiwani.
Kwa upande wa wanawake Tanzania Bara ni Zainab Rashid Mfaume Kawawa, Happyness Elias Lugiko, Fancy Haji Nkuhi, Happyness Ngoti Mgalula. Kwa wanaume Tanzania Bara ni pamoja na Dkt Ngwaru Jumanne Maghembe, Adamu Omari Kimbisa,Anamringi Issay Macha, Charles Makongoro Nyerere.
Kwa upande wa Zanzibar wanawake ni pamoja na Maryam Ussi Yahaya, Rabia Abdallah Hamid. Kwa wanaume Zanzibar Abdallah Hasnu Makame,Mohamedi Yusuph Nuh.
Pamoja na wagombea wote 12 bunge litapiga kura kwa kuchagua wabunge 6 watakaoiwakilisha Tanzania katika Bunge la Afrika Mashariki kwa tiketi ya chama hicho.

Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment