Diamond aizindua tovuti ya kuuzia muziki pinzani kwa Mkito


Tovuti namba moja ya kuuzia muziki nchini, Mkito.com, imepata mpinzani mpya, Wasafi.com. Diamond Platnumz ameizindua rasmi website yake ya kuuzia muziki, si tu wa wasanii wa WCB, bali wasanii wengine pia.


Wiki hii, hitmaker huyo wa Marry You, amekuwa akifanya mikutano ofisini kwake na wasanii mbalimbali, kuzungumza namna ya kufanya nao kazi kwenye mradi huo. Tayari amekutana na wasanii kama Ben Pol, Barnaba, Cassim pamoja na Chege na Temba.
Kwa mwelekeo huo, Wasafi.com inakuja kuwa mpinzani mkubwa wa Mkito.com, ambayo hadi sasa ndio website inayotegemewa na wasanii wengi kuuzia nyimbo zao.
Msanii wa WCB, Harmonize anaachia wimbo wake mpya exclusively kupitia website hiyo inayokuja na app yake pia
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment