Diamond amtia moyo Makonda, ‘Ukiona mtoto analia sana ujue viboko vinamkolea’

Diamond Platnumz amemtia moyo mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kutokana na maneno yanayozungumzwa tangu alipoanzisha vita ya kupambana na madawa ya kulevya.


Hitmaker huyo wa Marry You amesema hayo wakati alipoalikwa Jumatano hii kwenye sherehe za mwaka mmoja wa kumpongeza mkuu huyo wa mkoa tangu alipoteuliwa na Rais Magufuli kuwa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam. “Ukiona mtoto analia sana ujue viboko vinamkolea, kabisa. Hivyo ukiona maneno yanakuwa mengi ina maana kampeni inafanikiwa na sisi lengo letu kampeni ifanikiwe,” amesema Diamond.
Wakati huo huo muimbaji huyo amempongeza TID kwa kitendo chake cha kusimama mbele za watu na kukiri kuwa alikuwa anatumia madawa ya kulevya na kuahidi kuachana nayo.
“Kwanza nimpongeze kaka yangu TID, kwa sababu unapokuwa mwanamuziki ukasimama mbele za watu ukasema mimi nilikuwa nafanya lakini sasa hivi nimekuja katika njia nzuri ni kitu cha kumpongeza sana. Na mimi naamini kabisa ngoma yangu itakayotoka na TID itakuwa ngoma kubwa sana,” amesisitiza.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment