Diamond: Sina tatizo na Alikiba ni mtu ambaye ninaheshimiana naye

Diamond amethibitisha kuwa anamheshimu Alikiba na hana tatizo naye.

Hitmaker huyo wa Marry You amesema hayo Jumanne hii wakati alipokuwa akihojiwa katika kipindi cha Clouds 360 cha Clouds TV.


“Mimi sina tatizo na Alikiba ni mtu ambaye ninaheshimiana naye. Nimemfahamu kupitia dada yangu Queen Darleen,” amesema Diamond.
“Nilikutana na jamaa Nairobi tukazungumza naye maneno yapo yanasemwwa na watu katikati baadhi baadhi ya media wanachochea tu. Sijawahi kuwa na matatizo naye ni chokochoko tu za watu, menejimenti yangu pia inajaribu kuongea na wao waje kuuza muziki wao kwetu,” ameongeza.

Muimbaji huyo amesisitiza kuwa Joseph Kusaga ni mmoja kati ya watu ambao wanatamani kuona akifanya kazi pamoja na Kiba na sio kuchonganishwa ili kuwepo na uhasama kati yao.Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment