EFM yapewa ruksa ya kuruka mikoa 10 ya Tanzania, Nape amsifu Majay kwa uwekezaji mkubwa

Baada ya kufanya vizuri na kupata mashabiki wengi katika mji wa Dar es Salaam na Pwani, kituo cha redio cha EFM sasa kimepanua matangazo yake ambapo kinaanza kusikilizwa katika mikoa mingine tisa ya Tanzania.
Picha ya Majay wakwanza kushoto, akifuatiwa na waziri Nape, watatu ni mkurugenzi wa habari maelezo Hassan Abbas na mkurugenzi wa TCRA Francis Ntobi
Akiongea mbele ya mgeni rasmi ambaye ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye kwa niaba ya mkurugenzi wa EFM na TVE, General Manager wa EFM, Dennis Ssebo amesema TCRA imeipa kipali kituo hicho kuanza kurusha matangazo yake kwenye mikoa tisa ya Tanzania.
“Mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) imeipa kibali EFM kwenda mikoani na tunaingia kwenye mikoa tisa. Hiyo ndio habari kubwa ambayo mkurugenzi wa EFM alitaka kuzungumza na wananchi hii leo ni kwamba tumepewa ridhaa ya kwenda kwenye mikoa tisa. Mikoa hiyo ni ifuatayo Mbeya, Tanga, Mwanza, Mtwara, Manyara, Singida, Kigoma Tabora na Kilimanjaro.”

Mkurugenzi wa EFM na TVE, Majay akiongea na mkurugenzi wa TCRA Ntobi na mkurugenzi wa habari maelezo Hassan Abbas

Ntuli ambaye ni kiongozi wa upande wa production TVE akimuelekeza jambo mhe. Nape
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment