Jeshi la polisi ladaiwa kumshikilia Vanessa Mdee kwa tuhuma za kujihusisha na dawa za kulevya

Jeshi la Polisi jijini Dar es Salaam limemshikilia muimbaji Vanessa Mdee maarufu kama Vee Money kwa tuhuma za kujihusisha na dawa za kulevya.


Mwanasheria wake, Aman Tenga ametihibitisha kuwa mteja wake amejisalimisha mwenyewe Kituo Kikuu cha Polisi, kama ilivyoagizwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda wakati akitaja majina ya wanaojihusisha biashara hiyo pamoja na watumiaji mapema mwezi uliopita.
Mwanasheria Tenga pia ametihibitisha kuwa Vanessa alikuwa Afrika Kusini kikazi wakati jina lake likitajwa na Mkuu wa Mkoa. Pia aliongeza kuwa Polisi walikwenda Nyumbani kwa Vanessa kufanya upekuzi kabla ya kumpeleka kwa Mkemia Mkuu wa serikali kwa uchunguzi zaidi.
Vanessa Mdee ni Mtanzania wa kwanza kuwa mtangazaji wa MTV VJ, Mdee, alizaliwa mwaka 1988 Arusha, alianza kufahamika zaidi mara baada ya kutangaza kwenye Redio na Luninga kwenye vipindi kama Epic Bongo Star Search na Dume Challenge na baadae kidogo wakati ananza kujikita kwenye muziki alikuwa chini ya Lebo B’hitts.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment