Kigwangalla ainyooshea mikono ‘Marry You’ ya Diamond na Ne-Yo

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangalla ameonekana kuvutiwa na wimbo mpya wa Diamond ‘Marry You’ ambao amemshirikisha Ne-Yo kutoka Marekani

Kiongozi huyo kupitia mtandao wa Twitter amesema kuwa hajawahi kuwa shabiki wa Diamond lakini anazipenda nyimbo nne za muimbaji huyo huku akionekana kuunyooshea mikono wimbo wa ‘Marry You’ ambao mpaka sasa umefanikiwa kutazamwa mara milioni tano kwenye mtandao wa YouTube.
Sikuwahi kuwa mshabiki wa @diamondplatnumz, japokuwa ni mwimbaji mzuri, ila nakubali sana kipaji chake kwny ‘biashara’ ya muziki. Zaidi ya nyimbo ya @diamondplatnumz Mbagala (ambayo naipenda mpaka kesho), na juzi hapa nyimbo za Ngololo, Salome, hii ya #MarryYou 🙌🏾
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment