Kukaa magereza kumenipa ujasiri mkubwa na kumenisaidia kujua shida za watu -Lema

Mbunge wa Arusha Mjini (CHADEMA), Godbless Lema, amesema kuwa kukaa magereza kumempa ujasiri mkubwa na kumesaidia kujua shida za watu huku akisema kuwa kuna watu wamefungwa kwa kukutwa na mirungi

Mbunge huyo ameyasema hayo Ijumaa hii mbele ya maelfu ya wakazi wa Jiji la Arusha waliojitokeza katika mkutano wake wa kwanza tangu atoke gerezani, kwa dhamana.
“Ndugu zangu kukaa magereza kumenipa ujasiri mkubwa na kumesaidia kujua shida za watu, kwani kuna watu wamefungwa maisha kwa kukutwa na mirungi wakati nchi jirani Serikali inatoa fedha kupanua mashamba ya mirungi,” alisema lema.
Machi 3, mwaka huu, Lema aliachiwa kwa dhamana baada ya kukaa gerezani miezi minne tangu alipokamatwa akiwa bungeni mjini Dodoma, Novemba mwaka jana.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment