Mama Mlezi wa Rais Mstaafu Kikwete afariki dunia

Mbunge wa Jimbo la Chalinze na mtoto wa Rais mstaafu wa Tanzania wa awamu ya nne, Ridhiwani Kikwete kupitia ukurasa Instagram, ameandika ujumbe kuwa anasikitika kutangaza kifo cha bibi yake Bi. Nuru Khalfan Kikwete.Kwa mujibu wa Ridhiwani, kifo hicho kimechotokea asubuhi hii katika hospitali ya Muhimbili alipokuwa amelazwa kwa matibabu.

“TANZIA Ndugu na Marafiki nasikitika kuwatangazia Msiba/Kifo cha Bibi Yetu Bi.Nuru Khalfan Kikwete Kilichotokea asubuhi hii katika Hospitali ya Muhimbili alipokuwa amelazwa kwa Matibabu. Taratibu za mazishi tutajulishana . Innallilllah wainnaillah rajuun.#” ameandika kupitia ukurasa huo.


Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment