Mwakyembe aagiza Nay wa Mitego kuachiwa, aongelea ushauri wa JPM kwa Nay

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe, ameliagiza Jeshi la Polisi kumuachia huru Msanii Ney wa Mitego ambaye alikuwa akishikiliwa na Jeshi hilo.

Waziri Mwakyembe ameishauri pia BASATA kuondoa zuio lake dhidi ya wimbo wa ‘WAPO’ na badala yake uendelee kupigwa tu kama nyimbo nyingine.
Akiongea na Wandishi wa Habari Dodoma, Dk. Mwakyembe amesema hata Rais Magufuli amefurahishwa na wimbo huo wa WAPO na kumshauri Msanii huyo kama inawezekana aendelee kutaja watu wengine kama vile wakwepa Kodi, wauza Unga, wanaotumia dawa za kulevya pamoja na watu wengine wasio na maadili mema katika jamii.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment